maporomoko

maporomoko

Friday, October 12, 2012

RPC WA MKOA WA MWANZA LIBERATUS BARO AUAWA KWA KUPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI.

Taarifa zimeeleza kuwa kamanda baro aliuawa akiwa katika utekelezaji wa majukumu yake ya kifamilia ambapo imedaiwa kuwa alikuwa ameenda kuudhuria harusi na alipofika katika eneo harusi hiyo ilikokuwa ikifanyika wakati akishuka kwenye gari yake zilizuka prukushani ambazo bado waanzilishi na chanzo chake havijaelezwa na hivyo kupelekea kupigwa risasi ya kichwa na watu wanao sadikiwa kuwa ni majambazi.

tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo katika hoteli ya taifaivu iliyoko eneo la kitangile wilayani ilemela kilometa 1 moja kutoka barabara ya makongoro itokayo ilemela kuelekea mjini.

taarifa za kifo cha kamanda balo zimezibitishwa na msemaji wa jeshi la polisi tanzania hata hivyo blog hii makini itazidi kukuletea taarifa kadha zinazo husiana na sababu za kifo cha kamanda huyo kadri wasemaji wa jeshi la polisi watakavyo kuwa wakielezea kutokana na uchunguzi wao.

kamanda



Wednesday, October 10, 2012

Mauaji ya Daudi Mwangosi: Taarifa ya Tume ya Haki za Binadamu

 
Picture
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri Ramadhan Manento akionyesha taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa.


MUHTASARI WA TAARIFA YA TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA YA UCHUNGUZI WA TUKIO LILILOPELEKEA KIFO CHA DAUDI MWANGOSI KILICHOTOKEA SEPTEMBA 2, 2012 KIJIJINI NYOLOLO, WILAYA YA MUFINDI, MKOANI IRINGA


  1. UTANGULIZI
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (THBUB) ni idara huru ya serikali iliyoundwa kwa mujibu wa Kifungu cha 129(1)(c) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7  ya mwaka 2001. Jukumu kubwa la Tume ni kulinda, kutetea na kuhifadhi haki za binadamu nchini.  Katika kutekeleza jukumu hilo Tume imepewa mamlaka ya kupokea malalamiko (kwa njia mbalimbali) kutoka kwa mtu yeyote au kuanzisha uchunguzi wake yenyewe endapo itaona kuna uvunjifu wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


Kwa kuzingatia majukumu hayo, Tume ilianzisha uchunguzi wake yenyewe baada ya vyombo vya habari kutoa taarifa ya tukio la kifo cha Daudi Mwangosi. Tume iliunda timu ya watu watatu iliyoongozwa na Mhe. Kamishna Bernadeta Gambishi akisaidiwa na maafisa wawili, Bwana Gabriel Lubyagila na Bwana Yohana Mcharo. Timu hiyo ilifanya uchunguzi wake kuanzia tarehe 13-19 Septemba, 2012.


Katika uchunguzi uliofanywa, Tume ilizingatia zaidi masuala ya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora. Hivyo basi, Tume ilitilia maanani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, sheria mbalimbali za nchi na mikataba ya kimataifa na ya kikanda inayohusu haki za binadamu ambayo Tanzania imeridhia.


Kwa kuzingatia matakwa ya sheria ya Tume Na. 7 ya mwaka 2001, baada ya uchunguzi huo kukamilika, Tume imeandaa taarifa yake na kuiwasilisha kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.


Taarifa ya uchunguzi wa Tume imegawanyika katika sehemu kuu nne, ambazo ni:
    1. Maelezo ya viongozi, watendaji na wananchi waliohojiwa
    2. Uchambuzi wa taarifa/vielelezo vilivyopokelewa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu mbalimbali zinazohusiana na masuala ya haki za binadamu
    3. Matokeo ya uchunguzi
    4. Maoni na mapendekezo.


Kwa kuwa tukio la kifo cha Daudi Mwangosi liligusa hisia za jamii, Tume imeona ni vyema kukutana na wawakilishi wa vyombo vya habari  ili kutoa taarifa yake.


2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
Katika uchunguzi wake Tume imebaini kuwa:
    1. Tarehe 02/09/2012 Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiliruhusiwa na Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Mufindi (OCD) kufanya mikutano ya ndani na kuzindua matawi mapya.  Lakini jioni ya tarehe 01/09/2012 Kamanda wa Polisiwa Mkoa wa Iringa (RPC), alizuia CHADEMA kufanya mikutano iliyoruhusiwa na OCD ambaye ni Officer In-charge wa polisi wa eneo husika kama sheria inavyotaka.
    1. Viongozi wa CHADEMA walikuwa na mazungumzo na Mkuu wa Polisi Mkoa Upelelezi (RCO) na kuruhusiwa kufungua matawi yao bila ya kuwa na mikutano ya hadhara.
    1. Msajili wa vyama vya siasa aliwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa.
    1. Wakati shughuli za uzinduzi wa tawi la Nyololo ukiendelea, RPC alifika katika eneo hilo na kuamuru viongozi wa CHADEMA wakamatwe; na kuwa wafuasi wa CHADEMA walipingakukamatwa kwa viongozi wao.
    1. RPC aliamuru kupigwa kwa mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi waliokusanyika katika ofisi za tawi hilo la CHADEMA.
    1. Baada ya mabomu ya machozi kupigwa, wananchi walitawanyika na kukimbia ovyo; na kuwa marehemu Daudi Mwangosi alizingirwa na askari, aliteswa na hatimaye inadaiwaalipigwa bomu na kufa hapo hapo.
    1. Daudi Mwangosi aliuwawa umbali wa takriban mita 100 kutoka ilipo Ofisi ya CHADEMA tawi la Nyololo.
    1. Katika tukio hilo wananchi kadhaa walijeruhiwa kwa mabomu, wakiwemo Mwandishi wa Habari wa Nipashe, Bwana Godfrey Mushi, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake CHADEMA Wilaya ya Mufindi, Bibi Winnie Sanga na Mkuu wa Kituo cha PolisiMufindi, Asseli Mwampamba aliyekuwa akifanya jitihada zakumuokoa marehemu Daudi Mwangosi.


Kutokana na hayo yote, Tume imejiridhisha kuwa tukio lililopelekea kifo cha Daudi Mwangosi limegubikwa na uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


2.1 Uvunjwaji wa Haki za Binadamu
Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 1977, sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, Azimio la Kimataifa la Haki za Binadamu (Universal Declaration of Human Rights of 1948), Mkataba wa Kimataifa kuhusu haki za kiraia na kisiasa (International Covenant on Civil and Political Rights of 1966) na Mkataba wa mataifa ya Afrika kuhusu Haki za Binadamu na Watu (African Charter on Human and Peoples Rights of 1981), Tume imejiridhisha kuwa Jeshi la Polisi limevunja haki zifuatazo:
    • Haki ya kuishi,
    • Haki ya kutoteswa na kupigwa,
    • Haki ya usawa mbele ya sheria na
    • Haki ya kukusanyika na kutoa maoni.


CHADEMA ni chama cha siasa ambacho kina usajili wa kudumu.  Chini ya sheria ya vyama  vya siasa (Cap. 258 RE. 2002), vyama vya siasa vyenye usajili vimeruhusiwa kufanya maandamano na kuwa na mikutano ya kujitangaza baada ya kutoa taarifa kwa “Afisa wa Polisi” wa eneo husika.  Baada ya taarifa kutolewa chama husika kinatakiwa kipewe ulinzi na “security agencies” (mawakala wa usalama).

2.2 Ukiukwaji wa Misingi ya Utawala Bora
Ili pawepo utawala bora mamlaka zote za serikali ni lazima zifuate utawala wa sheria.  Uchunguzi umebaini kuwa kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda tarehe 02/09/2012 katika utekelezaji wa majukumu yake alikiuka Sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) kifungu cha 11(a) na (b) na sheria ya Polisi (Sura ya 322) kwa kuingilia kazi za OCD wa Mufindi na kutoa amri ya kuzuia shughuli za CHADEMA wakati yeye hakuwa “Officer In-charge” wa polisi wa eneo husika. Kwa maana hiyo amri aliyoitoa haikuwa halali kwa kuwa ilitolewa na mtu ambaye hakuwa na mamlaka kisheria kutoa amri hiyo.  Haya ni matumizi mabaya ya mamlaka, hivyo ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora.


Aidha, hatua ya Msajili wa vyama vya siasa, Mhe. John Tendwa kuwaandikia barua viongozi wa vyama vya siasa kuwataka kusitisha shughuli zao kwa sababu ya sensa ilikiuka misingi ya utawala bora kwani maelekezo yaliyotolewa ndani ya barua hizo yanakinzana na sheria ya takwimu Na. 1 ya mwaka 2002 inayotoa fursa kwa wananchi kuendelea na kazi zao wakati wa sensa pia ni kinyume na sheria ya vyama vya siasa (Cap 258 RE. 2002) Kifungu cha 11(a) na (b) inayotoa fursa kwa vyama vya siasa kufanya shughuli zake bila ya kuingiliwa.


Ibara ya 8(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaelezea kwamba Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya demokrasia na Haki ya Kijamii, aidha ibara 18(b) na (c) ya Katiba inaeleza kuwa kila mtu anayo haki ya kufanya mawasiliano (kutoa maoni/habari) na haki ya kutoingiliwa katika mawasiliano yake.  Haki hii imekiukwa kwa kiasi kikubwa na Jeshi la Polisi katika tukio la Nyololo Mufindi kwa kuwa waandishi wa habari na wafuasi wa CHADEMA walizuiwa na Polisi kufanya shughuli zao za kupata habari na za kisiasa.  Huu ni ukiukwaji wa misingi ya utawala bora kwa kuwa hali hiyo inazorotesha au inafifisha uhuru wa habari.

3.0 MAONI NA MAPENDEKEZO
Kwa kuzingatia Sheria ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Na. 7 ya mwaka 2001 Kifungu cha 15(2)(c) na 28 Tume inapendekeza yafuatayo:
    1. Kamati za ulinzi na usalama za Mkoa na Wilaya ziwe makini na vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wamisingi ya utalawa bora vinavyofanywa na mamlaka mbalimbali kwenye maeneo yao.  Aidha, kamati hizo zihusike moja kwa moja na usalama wa wananchi na mali zao kwa kujadili masuala yote ya kiusalama kabla hatua hazijachukuliwa na vyombo vinavyotekeleza sheria.
    1. Viongozi wa CHADEMA na wafuasi wao waepuke malumbano na vyombo vya dola kwa kutii maagizo yanayotolewa navyombo hivyo bila shuruti.  Pale wanapogundua kuwa pana uonevu au upendeleo ni vyema busara ikatumika ili kuepusha madhara makubwa yanayoweza kutokea.
    1. Jeshi la Polisi na Msajili wa Vyama vya Siasa waepuke kufanya maamuzi au matendo yanayoibua hisia za ubaguzi auupendeleo miongoni mwa jamii wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kisheria. Mfano, Jeshi la Polisi lilizuia mikutano ya CHADEMA kwa sababu ya sensa wakati huo huoChama cha Mapinduzi (CCM) walikuwa wakifanya uzinduzi wa Kampeni huko Zanzibar.  Aidha, rai ya Msajili wa vyama vya siasa haikuzingatiwa kwa upande wa CCM Zanzibar huku CHADEMA walishurutishwa na Polisi kutii rai hiyo.
    1. Demokrasia ya mfumo vya vyama vingi iheshimiwe na kulindwa.
    1. Elimu ya vyama vya siasa na sheria ya Polisi kuhusu vyama vya siasa itolewe kwa askari polisi ambao wanaonekana kutozifahamu kabisa.


4.0 HITIMISHO
Jukumu la kulinda amani na utulivu ni wajibu wa kila mtanzania, mkulima na mfanyakazi, viongozi wa serikali na watumishi wa umma wote wanapaswa kuwa wazalendo wa kweli wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.  Tume inatoa wito kwa watanzania wote kuheshimu haki za binadamu na kutekeleza kwa vitendo misingi ya utalawa bora.  Kwa kufanya hivi Taifa letu litaendelea kuwa na amani na utulivu.  Tume inatoa rai kwa jeshi la polisi kutekeleza wajibu wake mkuu wa ulinzi na usalama wa raia bila kutumia jazba.


Kuwepo kwa vyama vya siasa ionekane kuwa ni kukuwa kwa demokrasia na sio kuwa ni upinzani kwa chama tawala.


....................................................
Jaji Kiongozi (Mstaafu) Amiri R. Manento


MWENYEKITI
TUME YA HAKI ZA BINADAMU NA UTAWALA BORA


OKTOBA 10, 2012
Picture
Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mahfoudha.A. Hamid akijibu moja ya Swali kutoka kwa Mwandishi wa Habari (hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam kuhusu Muhtasari wa wa Taarifa ya tume yake ya Uchunguzi wa tukio lililopelekea kifo cha Mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten Daudi Mwangosi kilichotokea Septemba 2, 2012 kijijini Nyololo, Wilaya ya Mufindi, Mkoani Iringa. (Picha: Mwanakombo Jumaa-MAELEZO)

Tuesday, October 9, 2012

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,arejea hapa nchinibaada ya ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada.




 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akilakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kurejea nchini leo Jumanne Oktoba 10, 2012 akitokea katika ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akipokewa na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kurejea nchini leo Jumanne Oktoba 10, 2012 akitokea katika ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete,
akilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya
kurejea nchini leo Jumanne Oktoba 10, 2012 akitokea katika ziara ya
Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada.
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda, Waziri wa Sheria na Katiba Mhe Celina Kombani, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe Steven Wassira, Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Adama Malima na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Said Meck Sadiki katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kurejea nchini leo Jumanne Oktoba 9, 2012 akitokea katika ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada. (Picha: IKULU)
Picture
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, akiongea na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kurejea nchini leo Jumanne Oktoba 9, 2012 akitokea katika ziara ya Kikazi ya Marekani na Ziara Rasmi ya Kiserikali ya Canada.

Sunday, October 7, 2012


Sunday, October 7, 2012

SIR ALEX FERGUSON AMSIFIA DE GEA NA KUENDELEZA FOMULA YAKE YA KUBADIRISHA MAKIPA KILA MECHI!

Ingawa Sir Alex Ferguson amemsifia Kipa wake David De Gea kwa kudaka vizuri kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI hivi juzi katikati ya Wiki walipocheza huko Romania na CFR Cluj na kushinda bao 2-1, Meneja huyo wa Manchester United amesema ataendelea kuwabadili Makipa katika Mechi zijazo.
De Gea, Miaka 21, aliejiunga na Man United Msimu uliopita, aliachwa baada ya kucheza Mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu England Msimu huu na namba yake kupewa Anders Lindegaard, Miaka 28, kwenye Mechi 4 za Ligi ingawa De Gea alirudi tena na kucheza Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na CAPITAL ONE CUP dhidi ya Newcastle.
Mechi ijayo ya Man United ni ile ya Ligi Jumapili huko Sport Direct Arena ambapo wataivaa Newcastle na ni juu ya Ferguson kuamua amchezeshe Kipa toka Spain De Gea au Lindegaard kutoka Denmark.
Kuhusu hilo, Ferguson ametamka: “Yeye De Gea alicheza vyema na Cluj, ni Kipa mzuri sana, bado Kijana na anazidi kuimarika. Sijajua kama nitamchezesha yeye au la lakini tulichokuwa tukifanya katika Wiki chache zilizopita kimeenda vyema.”
Aliongeza: “Kila Mtu anataka kucheza na Makipa sio tofauti. Lakini ninachotizama sasa ni kuwapa uzoefu wote kitu ambacho kitatusaidia katika malengo ya muda mrefu. Ni wazi utafika wakati mmoja wao ndio atakuwa Namba wani akionyesha uimara mfululizo na akikomaa. Kwa sasa wote bado hawana uzoefu wa Mechi kubwa kabisa. Na hilo watalipata baada ya muda!”
Akizungumzia Makipa kucheza wakiwa na umri mkubwa, Ferguson alimtaja Kipa wake Edwin van der Sar aliestaafu Mwaka 2011 akiwa na Miaka 40 na akaongeza: “Peter Schmeichel alikuwa na Miaka 27 alipojiunga nasi na kila Mtu alimzungumzia kuwa ni Kijana wakati alikuwa na Miaka 27 lakini alitupa Miaka 8 ya uchezaji bora. Makipa wanaweza kucheza hata wakiwa na umri mkubwa sana wa kukaribia Miaka 40. Mtazame Brad Friedel, na Peter Shilton kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1990, alikuwa na Miaka 40!”

MOURINHO: NINA FURAHA TELE REAL MADRID ... SIONDOKI HADI NIMALIZE MKATABA MWINGINE NILIOSAINI WA MIAKA MINNE ... BAADA YA HAPO NAWEZA KURUDI ENGLAND..!


Mourinho

Mzee wa Mataji... Mourinho
MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa ana furaha tele katika klabu yake inayoshikilia ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kwamba hafikirii kuondoka kabla ya kumalizia mkataba mwingine mpya aliosaini hivi karibuni wa kubaki klabuni hapo kwa miaka minne zaidi.

Mourinho ametoa ufafanuzi huo kufuatia uvumi uliotanda kwamba yuko mbioni kurudi kufundisha katika klabu za Ligi Kuu ya England.
“Nina furaha na ninataka kubaki hapa. Nimesaini mkataba mwingine na Real Madrid utakaonibakiza kwa miaka mingine minne, ni kwa sababu sisi ni klabu bora zaidi duniani.

“Kufuatia mataji niliyotwaa England na Italia, Real Madrid ilikuwa inakosekana katika CV yangu. Na sasa kwa sababu tayari ninayo, ninapaswa kufanya kazi kwa uwezo wangu wote.
“Hata hivyo nilikuwa na furaha sana jijini London, na nitarudi tu.”


XAVI: NITAFURAHI SANA NIKIPIGA HAT-TRICK DHIDI YA REAL


Xavi
BARCELONA, Hispania
Kiungo nyota wa Barcelona, Xavi amesema kwamba kufunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi yao ya kesho Jumapili dhid ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid itakuwa ni furaha ya aina yake kwani ni ndoto itakayogeuka kuwa kweli

Nyota huyo mwenye miaka 32 ameshatwaa mataji kadhaa katika ngazi zote za klabu na timu ya taifa, lakini bado anasubiri kufunga hat-trick yake ya kwanza masihani, na anaona kuwa mechi ya kesho ya 'el clasico' itakuwa ni ndoto ya kweli pindi ikitokea akafunga kweli mabao matatu peke yake.

"Kuna kitu kingine ambacho bado sijafanya? Ni kufunga hat trick... nitafurahi sana nikipiga hat-trick yangu ya kwanza dhidi ya Real Madrid," Xavi amesema huku akitabasamu kwenye mkutano na waandishi wa habari.

"Kwakweli hatudhani kwamba ushindi dhjidi yao utazidi kuongeza migogoro ndani ya kikosi cha Real Madrid. Tumedhamiria kupata ushindi, jambo ambalo litatuongezea morari kikosini."

Kiungo huyo mchezeshaji ameendelea pia kuzungumzia hali ya majeruhi kikosini mwao kama Gerard Pique, Carles Puyol na Eric Abidal, ambaye afya yake inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa ini mwanzoni mwa mwaka huu.

"Hivi sasa, kuna nafasi ya asilimia 50 kwamba Pique atacheza dhidi ya Madrid," Xavi amesema.

"Jeraha la Puyol linasikitisha sana... yeye ni mfano ndani na nje ya uwanja kwa kila mchezaji na mara zote hucheza kwa nguvu zake zote.

"Abidal? Amehamasika sana kurejea kikosini."

Hivi sasa Barcelona wako klatika mazungumzo na wakala wa Xavi kuhusiana na mkataba wake mpya, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anaamini kwamba makubaliano yao yanasubiri muda tu.

"Nipo katika klabu bora zaidi duniani, ningependa kustaafu nikiwa hapa. Wakala wangu anazungumza na klabu kuhusiana na mkataba mwingine mpya, hakutakuwa na tatizo lolote," amesema Xavi.

ARSENAL YANG'ARA UGENINI NA KUSHINDA 3-1 DHIDI YA WEST HAM UNITED... CHELSEA YAIUA NORWICH CITY 4-1, MAN CITY YAIKANDAMIZA SUNDERLAND 3-0, WEST BROM 3 2 QPR


Sasa nd'o nimeanza safari ya kufunga mabao kama mvua ... Olivier Giroud wa Arsenal (katikati) akifunga dhidi ya West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Upton Park leo, Oktoba 6, 2012. (Picha: BBC)

Gooooh...! Fernando Torres akiifungia Chelsea bao la kusawazisha dhidi ya Norwich.

Nahodha Holt wa Norwich akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.

Safiiii... Torres wa Chelsea akipongezwa na wachezaji wenzake Juan Mata na Ivanovic baada ya kufunga goli lao la kusawazisha dhidi ya Norwich City leo.

Hazard wa Chelsea akifunga dhidi ya Norwich katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo.

Thomas Vermaelen wa Arsenal (kushoto) akichuana na Andy Carroll wa West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.
LONDON, England
Olivier Giroud alifunga goli lake la kwanza la Ligi Kuu ya England akiwa na Arsenal wakati 'Gunners' wakicharuka kutoka kuwa nyuma na kushinda ugenini kwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham jkwenye Uwanja wa Boleyn Ground, Upton Park jijini London usiku huu.

West Ham walipata goli la utangulizi kinyume na mwelekeo wa mechi katika dakika ya 21 wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Sengal, Mohamed Diame alipopiga shuti kali la 'upinde' lililomshinda kipa Vito Mannone na kujaa wavuni.

Giroud alisawazisha kabla ya mapumziko wakati alipoiwahi krosi ya Lukas Podolski na kuiunganishia wavuni, pembeni kwa ndani ya mlingoti wa goli.

Kevin Nolan
alikosa nafasi mbili za wazi kuwapa wenyeji uongozi na aliadhibiwa baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal bao la pili na mtokea benchi Theo Walcott aliyechukua nafasi ya Gervinho akaongeza goli la tatu wakati Arsenal wakicheza gonga safi huku West Ham wakionekana 'kutepeta'.

Giroud alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya England tangu atue Arsenal akitokea Ufaransa mwanzoni mwa msimu huu na kucheza kwa dakika 303 bila mafanikio. Goli hilo lilitokana na shuti lake la 12 (jumla 15, ukichanyanya na yaliyoyozuiwa) tangu aanze kucheza katika ligi kuu ya England.

Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Man City iliikandamiza Sunderland kwa mabao 3 - 0, Chelsea ikashinda 4-1 dhidi ya Norwich, Swansea na Reading zikatoka sare ya 2 - 2, West Brom wakazidi kuiweka pabaya Queen's Park Rangers kwa kuichapa mabao 3 - 2 na Wigan na Everton pia zikatoka sare ya 2 - 2.

HAPPY BIRTHDAY MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!

Tarehe ya leo Oktoba 7 ni siku aliyozaliwa Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho kikwete(JK). BUKOBASPORTS.COM inaungana na maelfu ya wananchi wa Tanzania na Duniani nzima waliomtakia maisha mema na wanaoendelea kumpongeza kwa siku hii. Sisi Bukobasports tunamtakia maisha marefu na ya afya njema na Mungu amjalie ili aweze kuliongoza Taifa letu vema.

Mc DONALD MARIGA AFUKUZIWA NA FULHAM, READING..!


MacDonald Mariga.
MacDonald Mariga wa Inter Milan akishangilia baada ya kufunga goli la tatu dhidi ya Genoa kuwania Kombe la Tim kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan,  Januari 12, 2011.
MILAN, Italia
Kiungo wa klabu ya Inter Milan inayoshiriki Serie A, Ligi Kuu ya Italia, Mkenya  McDonald Mariga anafukuziwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zikiwamo za Fulham na Reading, imefahamika.
McDonald akifanya mazoezi
Gazeti la Tuttosport limesema leo kuwa Fulham na Reading zinajiandaa kumfukuzia kiungo huyo wa timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari.


Inadaiwa kuwa Inter imepokea ofa kadhaa za kumsajili kiungo huyo mwenye miaka 25, zikiwamo za Fulham na Reading.


KUHUSU Mc DONALD 
Born: April 4, 1987 (age 25), Nairobi
Height: 1.88 m
Weight: 86 kg
Salary: $700,000 EUR (2012)
Siblings: Victor Wanyama, Thomas Wanyama, Sylvester Wanyama, Mercy Wanyama
Parents: Noah Wanyama, Mildred Wanyama

MBWANA SAMATTA, TRESSOR MPUTU WATOSWA KATIKA ORODHA YA NYOTA 34 WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA 2012... WAMEJAA 'MAPROO' WA ULAYA KAMA YAYA TOURE, DEMBA BA, GERVINHO, PAPISS DEMBA CISSE ... WANAOCHEZA AFRIKA NI WATATU TU AMBAO NI MSAKNI WA ESPERANCE YA TUNISIA, RAINFORD KIDIABA NA STOPHILA SUNZU WA TP MAZEMBE YA DR CONGO


Mbwana Samatta

Tressor Mputu

Yaya Toure
CAIRO, Misri
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetaja majina ya awali ya wachezaji nyota 34 barani wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Mwaka 2012 ambamo ndani yake, wamejaa 'maproo' 29 wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika huku nyota wa TP Mazembe, Mtanzania Mbwana Samatta na Tressor Mputu wanaong'ara katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika wakikosekana kwenye orodha hiyo.

Miongoni mwa wanaocheza soka la kulipwa Ulaya ni mshindi wa tuzo hiyo msimu uliopita, kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya England, Yaya Toure, mastraika nyota wa Newcastle United -- Papiss Demba Cisse na Demba Ba na pia winga wa Arsenal, Gervinho..


Wachezaji watatu wanaocheza katika klabu za Afrika ni Wazambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu wanaoichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Youssef Msakni wa Esperance ya Tunisia.


Orodha kamili:
1.    Abdelaziz Barrada - Getafe (Hispania) na Morocco

2.    Adel Taarabt - Queens Park Rangers (England) na Morocco

3.    Alain Sibiri Traore - Lorient (Ufaransa) na Burkina Faso

4.    Alexander Song - Barcelona (Hispania) na Cameroon

5.    Andre 'Dede' Ayew - Marseille (Ufaransa) na Ghana

6.    Arouna Kone - Wigan (England) na Ivory Coast

7.    Aymen Abdennour - Toulouse (Ufaransa) na Tunisia

8.    Bakaye Traore - AC Milan (Italia) na Mali

9.    Cheick Tiote - Newcastle United (England) na Ivory Coast

10.    Christopher Katongo - Henan Construction (China) na Zambia

11.    Demba Ba - Newcastle United (England) na Senegal

12.    Didier Drogba - Shanghai Shenhua (China) na Ivory Coast

13.    Emmanuel Agyemang-Badu - Udinese (Italia) na Ghana

14.    Emmanuel Mayuka - Southampton (England) na Zambia

15.    Foxi Kethevoama - FC Astana (Kazakhstan) na Afrika ya Kati.

16.    Gervinho - Arsenal (England) na Ivory Coast

17.    Hilaire Momi - Le Mans (Ufaransa) na Afrika ya Kati.

18.    John Obi Mikel - Chelsea (England) na Nigeria

19.    John Utaka - Montpellier (Ufaransa) na Nigeria

20.    Kwadwo Asamoah - Juventus (Italia) na Ghana

21.    Moussa Sow - Fenerbahce (Uturuki) na Senegal

22.    Nicolas N'koulou - Marseille (Ufaransa) na Cameroon

23.    Papiss Demba Cisse - Newcastle United (England) na Senegal

24.    Pape Moussa Konate - FC Krasnodar (Urusi) na Senegal

25.    Pierre-Emerick Aubameyang - St Etienne (Ufaransa) na Gabon

26.    Rainford Kalaba - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

27.    Seydou Doumbia - CSKA Moscow (Urusi) na Ivory Coast

28.    Seydou Keita - Dalian Aerbin (China) na Mali

29.    Sofiane Feghouli - Valencia (Hispania) na Algeria

30.    Stoppila Sunzu - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

31.    Victor Moses - Chelsea (England) na Nigeria

32.    Yaya Toure - Manchester City (England) na Ivory Coast

33.    Younes Belhanda - Montpellier (Ufaransa) na Morocco

34.    Youssef Msakni - Esperance (Tunisia) na Tunisia