maporomoko

maporomoko

Sunday, September 2, 2012

ZIARA YA MHE. SAMWEL SITTA MKOANI KAGERA YAMFIKISHA KATIKA KITUO CHA UHAMIAJI CHA MTUKULA MPAKANI WILAYANI MISSENYI.

Mhe. Samwel Sitta Akiongea na Wananchi wa Mpakani Mtukula Wilayani Missenyi

Mhe. Sitta Akiongea na Watumishi wa Serikali Mpakani Mtukula

Jengo linalojengwa la Ofisi zote za Mpakani katika eneo la Mtukula
Mkuu wa Mkoa wa Kagera Akimsomea Taaarifa ya Mkoa Mhe. Alipowasili Ofisini Kwake tarehe 27/08/2012


Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mheshimiwa Samwel Sitta ambaye anafanya ziara yake mkoani Kagera jana tarehe 27/08/2012 alianza ziara yake  Mtukula mpakani mwa Tanzania na Uganda na kukagua miradi mbalimbali mpakani hapo pia na kuongea wananchi wa pande zote mbili katika mpaka huo. 

Mhe.  Sitta katika ziara yake mpakani Mtukula alitoa agizo kwa uongozi wa vijiji vya Mtukula pande zote Tanzania na Uganda kuweka utaratibu wa kutengeneza vibali ambavyo watendaji wa vijiji hivyo pande zote mbili  watakuwa wanagonga mihuli na kumruhusu  mwananchi kuvuka mpaka na kufanya shughuli zake na kurudi.

“Pamoja na kuongea na wananchi wa Mtukula Mhe. Sitta alitembelea na kukagua ujenzi wa jengo lmoja la kukusanyia ushuru ambalo llitakuwa na ofisi zote za ushuru na ukaguzi wa mpakani kwa pande zote mbili Tanzania na Uganda. Ujenzi wa jengo hilo unaendelea vizuri na linakaribia kumalizika ujenzi wake. 

Mhe.  Samweli Sitta pia aliwahakikishia wananchi wa mpaka wa Mtukula kuwa serikali imetenga shilingi bilioni kumi na mbili kwaajili kupeleka umeme katika mpaka huo wa Mtukula na vijiji vyote vinavyopatikana katika njia hiyo ya kuelekea Mtukula ifikapo mwezi Desemba mwaka huu.

Aidha katika hatua nyingine Mhe. Sitta alisistiza wajasiliamali ambao wanaendesha biashara zao ndogondogo katika eneo la mpakani Mtukula kuwekewa mazingira mazuri ya kufanyia biashara zao ili kujiinua katika hali zao za maisha.

Katika ziara hiyo ya Mheshimiwa Sitta mkoani  Kagera pamoja na kutembelea Wilaya ya Missenye (Mtukula) pia anaendelea na Ziara yake katika Wilaya za Karagwe, Kyerwa (Murongo) na Ngara (Kabanga) katika mipaka inayopakana na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mkoa wa Kagera unapakana na Nchi zote za Afrika Mashariki ambazo ni Uganda, Kenya (Ziwani, Burundi na Rwanda.
Imetolewa na:
Sylvester Raphael
Afisa Habari Mkoa,
Kagera @2012

No comments:

Post a Comment