maporomoko

maporomoko

Sunday, October 7, 2012


Sunday, October 7, 2012

SIR ALEX FERGUSON AMSIFIA DE GEA NA KUENDELEZA FOMULA YAKE YA KUBADIRISHA MAKIPA KILA MECHI!

Ingawa Sir Alex Ferguson amemsifia Kipa wake David De Gea kwa kudaka vizuri kwenye Mechi ya UEFA CHAMPIONS LIGI hivi juzi katikati ya Wiki walipocheza huko Romania na CFR Cluj na kushinda bao 2-1, Meneja huyo wa Manchester United amesema ataendelea kuwabadili Makipa katika Mechi zijazo.
De Gea, Miaka 21, aliejiunga na Man United Msimu uliopita, aliachwa baada ya kucheza Mechi mbili za kwanza za Ligi Kuu England Msimu huu na namba yake kupewa Anders Lindegaard, Miaka 28, kwenye Mechi 4 za Ligi ingawa De Gea alirudi tena na kucheza Mechi ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na CAPITAL ONE CUP dhidi ya Newcastle.
Mechi ijayo ya Man United ni ile ya Ligi Jumapili huko Sport Direct Arena ambapo wataivaa Newcastle na ni juu ya Ferguson kuamua amchezeshe Kipa toka Spain De Gea au Lindegaard kutoka Denmark.
Kuhusu hilo, Ferguson ametamka: “Yeye De Gea alicheza vyema na Cluj, ni Kipa mzuri sana, bado Kijana na anazidi kuimarika. Sijajua kama nitamchezesha yeye au la lakini tulichokuwa tukifanya katika Wiki chache zilizopita kimeenda vyema.”
Aliongeza: “Kila Mtu anataka kucheza na Makipa sio tofauti. Lakini ninachotizama sasa ni kuwapa uzoefu wote kitu ambacho kitatusaidia katika malengo ya muda mrefu. Ni wazi utafika wakati mmoja wao ndio atakuwa Namba wani akionyesha uimara mfululizo na akikomaa. Kwa sasa wote bado hawana uzoefu wa Mechi kubwa kabisa. Na hilo watalipata baada ya muda!”
Akizungumzia Makipa kucheza wakiwa na umri mkubwa, Ferguson alimtaja Kipa wake Edwin van der Sar aliestaafu Mwaka 2011 akiwa na Miaka 40 na akaongeza: “Peter Schmeichel alikuwa na Miaka 27 alipojiunga nasi na kila Mtu alimzungumzia kuwa ni Kijana wakati alikuwa na Miaka 27 lakini alitupa Miaka 8 ya uchezaji bora. Makipa wanaweza kucheza hata wakiwa na umri mkubwa sana wa kukaribia Miaka 40. Mtazame Brad Friedel, na Peter Shilton kwenye Fainali za Kombe la Dunia Mwaka 1990, alikuwa na Miaka 40!”

MOURINHO: NINA FURAHA TELE REAL MADRID ... SIONDOKI HADI NIMALIZE MKATABA MWINGINE NILIOSAINI WA MIAKA MINNE ... BAADA YA HAPO NAWEZA KURUDI ENGLAND..!


Mourinho

Mzee wa Mataji... Mourinho
MADRID, Hispania
Kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho amesema kuwa ana furaha tele katika klabu yake inayoshikilia ubingwa wa La Liga, Ligi Kuu ya Hispania na kwamba hafikirii kuondoka kabla ya kumalizia mkataba mwingine mpya aliosaini hivi karibuni wa kubaki klabuni hapo kwa miaka minne zaidi.

Mourinho ametoa ufafanuzi huo kufuatia uvumi uliotanda kwamba yuko mbioni kurudi kufundisha katika klabu za Ligi Kuu ya England.
“Nina furaha na ninataka kubaki hapa. Nimesaini mkataba mwingine na Real Madrid utakaonibakiza kwa miaka mingine minne, ni kwa sababu sisi ni klabu bora zaidi duniani.

“Kufuatia mataji niliyotwaa England na Italia, Real Madrid ilikuwa inakosekana katika CV yangu. Na sasa kwa sababu tayari ninayo, ninapaswa kufanya kazi kwa uwezo wangu wote.
“Hata hivyo nilikuwa na furaha sana jijini London, na nitarudi tu.”


XAVI: NITAFURAHI SANA NIKIPIGA HAT-TRICK DHIDI YA REAL


Xavi
BARCELONA, Hispania
Kiungo nyota wa Barcelona, Xavi amesema kwamba kufunga mabao matatu (hat-trick) katika mechi yao ya kesho Jumapili dhid ya mahasimu wao wa jadi, Real Madrid itakuwa ni furaha ya aina yake kwani ni ndoto itakayogeuka kuwa kweli

Nyota huyo mwenye miaka 32 ameshatwaa mataji kadhaa katika ngazi zote za klabu na timu ya taifa, lakini bado anasubiri kufunga hat-trick yake ya kwanza masihani, na anaona kuwa mechi ya kesho ya 'el clasico' itakuwa ni ndoto ya kweli pindi ikitokea akafunga kweli mabao matatu peke yake.

"Kuna kitu kingine ambacho bado sijafanya? Ni kufunga hat trick... nitafurahi sana nikipiga hat-trick yangu ya kwanza dhidi ya Real Madrid," Xavi amesema huku akitabasamu kwenye mkutano na waandishi wa habari.

"Kwakweli hatudhani kwamba ushindi dhjidi yao utazidi kuongeza migogoro ndani ya kikosi cha Real Madrid. Tumedhamiria kupata ushindi, jambo ambalo litatuongezea morari kikosini."

Kiungo huyo mchezeshaji ameendelea pia kuzungumzia hali ya majeruhi kikosini mwao kama Gerard Pique, Carles Puyol na Eric Abidal, ambaye afya yake inaendelea kuimarika baada ya kufanyiwa upasuaji wa kupandikiziwa ini mwanzoni mwa mwaka huu.

"Hivi sasa, kuna nafasi ya asilimia 50 kwamba Pique atacheza dhidi ya Madrid," Xavi amesema.

"Jeraha la Puyol linasikitisha sana... yeye ni mfano ndani na nje ya uwanja kwa kila mchezaji na mara zote hucheza kwa nguvu zake zote.

"Abidal? Amehamasika sana kurejea kikosini."

Hivi sasa Barcelona wako klatika mazungumzo na wakala wa Xavi kuhusiana na mkataba wake mpya, na mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania anaamini kwamba makubaliano yao yanasubiri muda tu.

"Nipo katika klabu bora zaidi duniani, ningependa kustaafu nikiwa hapa. Wakala wangu anazungumza na klabu kuhusiana na mkataba mwingine mpya, hakutakuwa na tatizo lolote," amesema Xavi.

ARSENAL YANG'ARA UGENINI NA KUSHINDA 3-1 DHIDI YA WEST HAM UNITED... CHELSEA YAIUA NORWICH CITY 4-1, MAN CITY YAIKANDAMIZA SUNDERLAND 3-0, WEST BROM 3 2 QPR


Sasa nd'o nimeanza safari ya kufunga mabao kama mvua ... Olivier Giroud wa Arsenal (katikati) akifunga dhidi ya West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England kwenye Uwanja wa Upton Park leo, Oktoba 6, 2012. (Picha: BBC)

Gooooh...! Fernando Torres akiifungia Chelsea bao la kusawazisha dhidi ya Norwich.

Nahodha Holt wa Norwich akishangilia baada ya kuifungia timu yake goli la kuongoza dhidi ya Chelsea wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.

Safiiii... Torres wa Chelsea akipongezwa na wachezaji wenzake Juan Mata na Ivanovic baada ya kufunga goli lao la kusawazisha dhidi ya Norwich City leo.

Hazard wa Chelsea akifunga dhidi ya Norwich katika mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo.

Thomas Vermaelen wa Arsenal (kushoto) akichuana na Andy Carroll wa West Ham wakati wa mechi yao ya Ligi Kuu ya England leo Oktoba 6, 2012.
LONDON, England
Olivier Giroud alifunga goli lake la kwanza la Ligi Kuu ya England akiwa na Arsenal wakati 'Gunners' wakicharuka kutoka kuwa nyuma na kushinda ugenini kwa mabao 3-1 dhidi ya West Ham jkwenye Uwanja wa Boleyn Ground, Upton Park jijini London usiku huu.

West Ham walipata goli la utangulizi kinyume na mwelekeo wa mechi katika dakika ya 21 wakati mshambuliaji wa kimataifa wa Sengal, Mohamed Diame alipopiga shuti kali la 'upinde' lililomshinda kipa Vito Mannone na kujaa wavuni.

Giroud alisawazisha kabla ya mapumziko wakati alipoiwahi krosi ya Lukas Podolski na kuiunganishia wavuni, pembeni kwa ndani ya mlingoti wa goli.

Kevin Nolan
alikosa nafasi mbili za wazi kuwapa wenyeji uongozi na aliadhibiwa baada ya Santi Cazorla kuifungia Arsenal bao la pili na mtokea benchi Theo Walcott aliyechukua nafasi ya Gervinho akaongeza goli la tatu wakati Arsenal wakicheza gonga safi huku West Ham wakionekana 'kutepeta'.

Giroud alifunga goli lake la kwanza katika ligi kuu ya England tangu atue Arsenal akitokea Ufaransa mwanzoni mwa msimu huu na kucheza kwa dakika 303 bila mafanikio. Goli hilo lilitokana na shuti lake la 12 (jumla 15, ukichanyanya na yaliyoyozuiwa) tangu aanze kucheza katika ligi kuu ya England.

Katika mechi nyingine zilizochezwa leo, Man City iliikandamiza Sunderland kwa mabao 3 - 0, Chelsea ikashinda 4-1 dhidi ya Norwich, Swansea na Reading zikatoka sare ya 2 - 2, West Brom wakazidi kuiweka pabaya Queen's Park Rangers kwa kuichapa mabao 3 - 2 na Wigan na Everton pia zikatoka sare ya 2 - 2.

HAPPY BIRTHDAY MHESHIMIWA RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE!!!

Tarehe ya leo Oktoba 7 ni siku aliyozaliwa Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Mrisho kikwete(JK). BUKOBASPORTS.COM inaungana na maelfu ya wananchi wa Tanzania na Duniani nzima waliomtakia maisha mema na wanaoendelea kumpongeza kwa siku hii. Sisi Bukobasports tunamtakia maisha marefu na ya afya njema na Mungu amjalie ili aweze kuliongoza Taifa letu vema.

Mc DONALD MARIGA AFUKUZIWA NA FULHAM, READING..!


MacDonald Mariga.
MacDonald Mariga wa Inter Milan akishangilia baada ya kufunga goli la tatu dhidi ya Genoa kuwania Kombe la Tim kwenye Uwanja wa Giuseppe Meazza mjini Milan,  Januari 12, 2011.
MILAN, Italia
Kiungo wa klabu ya Inter Milan inayoshiriki Serie A, Ligi Kuu ya Italia, Mkenya  McDonald Mariga anafukuziwa na klabu kadhaa za Ligi Kuu ya England zikiwamo za Fulham na Reading, imefahamika.
McDonald akifanya mazoezi
Gazeti la Tuttosport limesema leo kuwa Fulham na Reading zinajiandaa kumfukuzia kiungo huyo wa timu ya taifa ya Kenya 'Harambee Stars' wakati wa dirisha dogo la usajili wa Januari.


Inadaiwa kuwa Inter imepokea ofa kadhaa za kumsajili kiungo huyo mwenye miaka 25, zikiwamo za Fulham na Reading.


KUHUSU Mc DONALD 
Born: April 4, 1987 (age 25), Nairobi
Height: 1.88 m
Weight: 86 kg
Salary: $700,000 EUR (2012)
Siblings: Victor Wanyama, Thomas Wanyama, Sylvester Wanyama, Mercy Wanyama
Parents: Noah Wanyama, Mildred Wanyama

MBWANA SAMATTA, TRESSOR MPUTU WATOSWA KATIKA ORODHA YA NYOTA 34 WANAOWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA AFRIKA 2012... WAMEJAA 'MAPROO' WA ULAYA KAMA YAYA TOURE, DEMBA BA, GERVINHO, PAPISS DEMBA CISSE ... WANAOCHEZA AFRIKA NI WATATU TU AMBAO NI MSAKNI WA ESPERANCE YA TUNISIA, RAINFORD KIDIABA NA STOPHILA SUNZU WA TP MAZEMBE YA DR CONGO


Mbwana Samatta

Tressor Mputu

Yaya Toure
CAIRO, Misri
Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) limetaja majina ya awali ya wachezaji nyota 34 barani wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika Mwaka 2012 ambamo ndani yake, wamejaa 'maproo' 29 wanaocheza soka la kulipwa nje ya Afrika huku nyota wa TP Mazembe, Mtanzania Mbwana Samatta na Tressor Mputu wanaong'ara katika Ligi ya Klabu Bingwa Afrika wakikosekana kwenye orodha hiyo.

Miongoni mwa wanaocheza soka la kulipwa Ulaya ni mshindi wa tuzo hiyo msimu uliopita, kiungo wa timu ya taifa ya Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya England, Yaya Toure, mastraika nyota wa Newcastle United -- Papiss Demba Cisse na Demba Ba na pia winga wa Arsenal, Gervinho..


Wachezaji watatu wanaocheza katika klabu za Afrika ni Wazambia Rainford Kalaba na Stoppila Sunzu wanaoichezea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Youssef Msakni wa Esperance ya Tunisia.


Orodha kamili:
1.    Abdelaziz Barrada - Getafe (Hispania) na Morocco

2.    Adel Taarabt - Queens Park Rangers (England) na Morocco

3.    Alain Sibiri Traore - Lorient (Ufaransa) na Burkina Faso

4.    Alexander Song - Barcelona (Hispania) na Cameroon

5.    Andre 'Dede' Ayew - Marseille (Ufaransa) na Ghana

6.    Arouna Kone - Wigan (England) na Ivory Coast

7.    Aymen Abdennour - Toulouse (Ufaransa) na Tunisia

8.    Bakaye Traore - AC Milan (Italia) na Mali

9.    Cheick Tiote - Newcastle United (England) na Ivory Coast

10.    Christopher Katongo - Henan Construction (China) na Zambia

11.    Demba Ba - Newcastle United (England) na Senegal

12.    Didier Drogba - Shanghai Shenhua (China) na Ivory Coast

13.    Emmanuel Agyemang-Badu - Udinese (Italia) na Ghana

14.    Emmanuel Mayuka - Southampton (England) na Zambia

15.    Foxi Kethevoama - FC Astana (Kazakhstan) na Afrika ya Kati.

16.    Gervinho - Arsenal (England) na Ivory Coast

17.    Hilaire Momi - Le Mans (Ufaransa) na Afrika ya Kati.

18.    John Obi Mikel - Chelsea (England) na Nigeria

19.    John Utaka - Montpellier (Ufaransa) na Nigeria

20.    Kwadwo Asamoah - Juventus (Italia) na Ghana

21.    Moussa Sow - Fenerbahce (Uturuki) na Senegal

22.    Nicolas N'koulou - Marseille (Ufaransa) na Cameroon

23.    Papiss Demba Cisse - Newcastle United (England) na Senegal

24.    Pape Moussa Konate - FC Krasnodar (Urusi) na Senegal

25.    Pierre-Emerick Aubameyang - St Etienne (Ufaransa) na Gabon

26.    Rainford Kalaba - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

27.    Seydou Doumbia - CSKA Moscow (Urusi) na Ivory Coast

28.    Seydou Keita - Dalian Aerbin (China) na Mali

29.    Sofiane Feghouli - Valencia (Hispania) na Algeria

30.    Stoppila Sunzu - TP Mazembe (DR Congo) na Zambia

31.    Victor Moses - Chelsea (England) na Nigeria

32.    Yaya Toure - Manchester City (England) na Ivory Coast

33.    Younes Belhanda - Montpellier (Ufaransa) na Morocco

34.    Youssef Msakni - Esperance (Tunisia) na Tunisia

No comments:

Post a Comment