maporomoko

maporomoko

Saturday, September 29, 2012

Rais Kikwete aonana na Ujumbe wa MWAPORC 29/09/2012 0 Comments Picture Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli.
  (picha:IKULU) Picture Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiuonesha njia za reli katika ramani ya Tanzania ujumbe toka kampuni ya Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka kuwekeza katika sekta ya reli. (picha: IKULU)

Thursday, September 27, 2012






JESHI la Polisi jana lilitumia nguvu kuwadhibiti waandishi wa habari wasimpige picha askari Namba G.2573, Pacificus Cleophase Simon (23) anayeshitakiwa kwa tuhuma za kumuua Mwandishi wa Habari wa Channel Ten, Daudi Mwangosi.

Katika harakati hizo, Mwandishi wa Habari wa Tanzania Daima, Gustav Chahe alinusurika kupata kipigo kutoka kwa makachero waliokuwepo m
UPDATES za maelezo, picha na video kutoka kwenye  “BLOGU YETU

Vurugu zimetokea jijini Arusha siku ya Alhamisi, September 27, 2012 kuanzia muda wa saa 2:32 asubuhi.

Awali, Mamlaka ya Seikali ya Jiji la Arusha iliwahamisha Wafanyabiashara ndogondogo waliokuwa maeneo tofauti katikati ya jiji la Arusha na kuwapeleka kwenye viwanja vya NMC.

Wafanyabiashara hao walikaa siku chache na wakaanzisha madai kuwa eneo hilo halina huduma za kijamii kama choo, maji, kivuli na pia kwamba eneo hujaa maji pindi mvua inyeshapo. Kutokana na hilo ndipo wafanya biashara hao wakaamua kuja eneo la Kilombero kuvunja uzio wa mabati kuzunguka eneo lenye mgogoro mahakamani ili walitumie kufanyia biashara zao.

Wamechoma moto matairi ndani ya eneo lililowekewa uzio wa mabati.

Walivamia na kuvunja uzio huo na kuanza kujigawia viwanja ila wafanyie hapo biashara zao.

Jitihada zinafanyika kutatua mgogoro huu haraka iwezekanavyo.

Hayo yanafanyika wakati Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete, Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Mataifa, Koffi Annan na wakuu wengine wapo Jijini Arusha katika mkutano wa Kimataifa.

(Bofya picha zilizopachikwa hapo kuzikuza)


Wednesday, September 19, 2012

Mwonekano wa baadhi ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Songambele iliyopo wilaya mpya ya Kyerwa mkoa wa Kagera kwa watu wanaoishi mjini huwezi kujua kama kwa miaka 50 ya uhuru kama bado kuna madarasa ya aina hii.

Hapa wanafunzi wapo darasani wakiendelea na masomo ingawa darasa mabovu lakini wana madawati.





Ofisi ya tawi ya chama cha mapinduzi CCM katika kata ya songambele ingawa kinaitwa kimetawala kwa miaka 50 bado majengo yake yako hivi.  





Sunday, September 16, 2012

Umma wa watanzania uliofurika LINAS kuwaangalia wasanii wa BONGO MOVIE AKINA JB,JACLINE na ANTIEZEKIEL lakini wakaambulia patupu baada ya mambo kuwa ZIRO PLUS ZIRO.pole sana mlioingizwa mkenge.

Hawa  ni miongoni mwa washiriki wa mchakato wa kutafuta Wasanii wa kuigiza filamu katika manispaa ya bukoba wakiingia ukumbini kwa mbwembwe zisizo za kisayansi.





Mkurugenzi mkuu wa Zachwa Investment Bw. Muganyizi (kulia) pamoja na Mr. Nyerere wanahusika .
DJ Slay (kulia) wa pili kutoka kulia ni  Bi.Jane Zachwa, anayefuata ni  Abera Kamara a.ka MALIKIA na mwisho ni  Bi.Jane Zachwa ambaye ndiye Chief Judge wa shindano hili huku hao wengine wakisaidiana naye katika shughuli nzima ya kuaji ijapo dukuduku lilitanda kwa umma uliofika kuchungulia shughuli hiyo kama majaji wana elimu kiduchu juu ya mambo ya sanaa mi SIMO hiyo ilikuwa minongono TU.BASATA kazi wanayo.
 Pamoja na majaji wengine
Washiriki wakicheza kwa woga huku wakitokwa kijasho juu ya nani atatemwa na nani atabebwa.

wakati wa kila mtu kujidadavua ukawadia.
kwa upande wa wadau wakachoka kusubiri kuwaona akiana JB bila mafanikio pozi za usingizi zikaanza kuwanyemerea.

Meza kuu ikajitaidi kuchangamsha ukumbi lakini haa wapi?


Bwana  Jamali Kalumuna a.k.a jamco akiwaza na kuwazua ni jinsi gani atawabwaga baadhi ya washiriki ambao vigezo vyao ni ziro.
group la  wasafi clasic la Kagera wakiwaza plani B baada ya kujitokeza mizengwe ya kutaka kuwachakachua elfu sitini malipo ya shoo yao.

burudani ilikuwepo ila siyo ile iliyo haidiwa kwahiyo bado mambo yalibaki kukwa...............
Baadae watu wakakubali yaishe.Hii ina maana gani? Picha za washindi tunakuletea hivi punde.usisign out.

Taarifa ya Naibu Waziri kuhusu mtihani wa kumaliza elimu ya Msingi, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI MWAKA 2012

 Ndugu wananchi,

Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi Tanzania Bara utafanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.  Jumla ya wanafunzi 894,881 wamesajiliwa  kufanya mtihani huo ambapo   wavulana ni  426,285 sawa na asilimia 47.64  na wasichana ni 468,596  sawa na asilimia 52.36. Aidha, kati ya  wanafunzi hao, wapo wanafunzi 874,379  watakaofanya mtihani huo kwa lugha ya Kiswahili na wanafunzi 20,502 watafanya kwa lugha ya Kiingereza ambayo ndiyo waliyoitumia kujifunzia.  Wanafunzi wasioona waliosajiliwa kufanya mtihani ni 92 wakiwemo wavulana 53 na wasichana 39.  Watahiniwa wenye uono hafifu ambao huhitaji maandishi makubwa ni 495, kati yao wavulana ni 238 na wasichana ni 257.

Mtihani huu utafanyika kwa mara ya kwanza kwa kutumia teknolojia mpya ya ‘Optical Mark Reader’ (OMR), ambapo watahiniwa watatumia fomu maalum za OMR kujibia mtihani na majibu yao yatasahihishwa kwa kutumia kompyuta.  Masomo yatakayotahiniwa katika mtihani huo ni Kiswahili, English Language, Sayansi, Hisabati na Maarifa ya Jamii.

Ndugu wananchi,

Maandalizi yote kwa ajili ya mtihani huo yamekamilika ikiwa ni pamoja na kusambazwa kwa karatasi za mitihani, kusambazwa kwa fomu maalum za   kujibia mtihani na nyaraka zote zinazohusu mtihani huo. Mafunzo maalum kwa ajili ya matumizi ya fomu za OMR yamefanyika kwa lengo la kuwaandaa watahiniwa, wasimamizi pamoja na viongozi wa elimu katika ngazi mbalimbali ili waweze kutumia ipasavyo teknolojia hiyo.

Ndugu wananchi,

Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi ni muhimu kwa wanafunzi na jamii kwa ujumla kwa kuwa unahitimisha ngazi ya Elimu ya Msingi na kufungua milango kwa ajili ya elimu ya sekondari.  Hivyo, matokeo ya mtihani huu hutumika katika uchaguzi wa wanafunzi wanaojiunga na Elimu ya Sekondari.   Kwa kuzingatia umuhimu wa mtihani huo, napenda kutumia fursa hii kutoa wito kwa Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa taratibu zote za mitihani zinazingatiwa ipasavyo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa  mazingira yanakuwa salama na tulivu na kuzuia mianya yote inayoweza kusababisha udanganyifu.

Napenda pia kutoa wito kwa wasimamizi wa mitihani kufanya kazi yao ya kusimamia kwa umakini na uadilifu wa hali ya juu.  Wapo baadhi ya wasimamizi ambao wamekuwa wakishiriki katika kuwasaidia watahiniwa kufanya udanganyifu kwenye mitihani.   Napenda kuwaasa tena wasimamizi kujiepusha na vitendo hivyo vya udanganyifu kwani serikali haitasita kuchukulia hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayebainika kukiuka taratibu za mitihani.

Kwa upande wa wanafunzi watakaofanya mtihani mwaka huu, ninaamini kuwa walimu wamewaandaa vizuri katika kipindi chote cha miaka saba ya Elimu ya Msingi.  Hivyo, ni matarajio yangu kuwa mtaufanya mtihani huo kwa utulivu na kuzingatia taratibu zote za mitihani ili matokeo ya mtihani yaoneshe uwezo wenu halisi kulingana na maarifa na ujuzi mliopata katika Elimu ya Msingi.  Serikali inawaasa wanafunzi wote kutojihusisha na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika mtihani kwani watakaobainika watafutiwa matokeo yao yote ya mtihani.

Ndugu wananchi,

Natoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano unaotakiwa katika kuhakikisha kwamba mtihani huo  unafanyika kwa amani na utulivu wa kutosha bila usumbufu unaoweza kusababishwa na shughuli za kijamii hasa katika maeneo ya jirani na shule.

Mwisho, napenda kuwaasa tena wanafunzi, walimu na wananchi wote kwa ujumla kujiepusha na vitendo vya udanganyifu wa aina yoyote katika Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi. Nawaomba pia raia wema wasisite kutoa taarifa katika vyombo husika pindi wanapoona au kuhisi mtu au kikundi cha watu kinajihusisha na udanganyifu wa aina yoyote katika mtihani huo.

Nawatakia watahiniwa wote heri na fanaka katika mtihani utakaofanyika tarehe 19 na 20 Septemba, 2012.

MHESHIMIWA PHILIPO AUGUSTINO MULUGO (MB)
NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

Monday, September 10, 2012

Mkutano wa Maandalizi ya Watalamu wa Nchi za Afrika wafanyika Mjini Arusha

Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akisalimiana na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bw Richad Muyungi alipowasili Kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Arusha ICC tayari Kufunguwa Mkutano wa Wataalamu wa Mazingira barani Afrika unaofayika Mjini Arusha.{Picha na Ali Meja]
Mkutano Umefuguliwa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa AICC Mjini Arusha.Baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Waatalamu wa Mazingira wa Nchi za Afrika Wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga (hayupo pichani) akifungua kikao cha Maandalizi ya Mkutano wa Mawaziri wa Mazingira Afrika, katika ukumbi wa AICC- Arusha.Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akifungua Mkutano wa Watalamu wa Mazingira wa Afrika kuhusu Maendeleo Endelevu Baada ya Mkutano wa Rio+20 Naibu 


picha kwa hisabi ya MICHUZI blog spot.

Majaribio ya Daladala-Treni ya ndani ya jiji la Dar es Salaam yaanza

Picture
Daladala Treni yaanza kufanya majaribio Dar es Salaam (picha Mwananchi Communications Ltd - facebook)
Picture
Kichwa cha treni pamoja na mabehewa sita ya awamu ya kwanza, yakisubiri kufanyiwa majaribio kwa Safari zitazoanzia Station Dar es Salaam mpaka Ubungo mnamo mwezi wa kumi, majaribia hayo yameongozwa asubuhi ya leo na Naibu Waziri wa Uchukuzi,Mhe. Dk Charles Tizeba (Mb) ambaye alipanda treni hiyo kuanzia Station Dar es Salaam Mpaka Ubungo.Serikali imetumia kiasi cha Sh. Bil 4.75 kwa ajili ya ukarabati wa njia, injini na mabehewa. (picha: Raha za Pwani Blog)
Picture
Baadhi ya Wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) wakiwa na furaha ndani ya mojawapo ya mabehewa yaliyofanyiwa majaribio leo abubuhi. (picha: Raha za Pwani Blog)
Picture
Naibu Waziri wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Charles Tizeba (Mb) dirisha la pili kutoka kulia, akiangalia nje wakati wa majaribio ya mabehewa sita kati ya kumi na mbili yatakayofanya safari zake kutoka Station mpaka Ubungo kuanzia mwezi wa Kumi mwaka huu,Treni hizo zitasaidia wananchi katika usafiri jijini Dar es Salaam. (picha: Raha za Pwani Blog)

Thursday, September 6, 2012

RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO LA KIMATAIFA LA KILIMO


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS KIKWETE ATUNUKIWA TUZO LA KIMATAIFA LA KILIMO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Tuzo Maalum ya Sera za Usalama wa Chakula na Uongozi Katika Sekta ya Kilimo ikiwa ni ishara ya kuthamini mchango wake na uongozi wake katika sekta hiyo ya kilimo.

Tuzo hiyo imetolewa na Taasisi ya Mtandao wa Kutathmini Sera za Kilimo na Maliasili – Agriculture and Natural Resources Policy Analysis Network (FANRPAN) katika hafla maalum iliyofanyika jioni ya jana, Jumatano, Septemba 5, 2012, wakati wa  mkutano wake wa mwaka unaofanyika kwenye Hoteli ya White Sands mjini Dar es Salaam.

Rais Kikwete anakuwa kiongozi wa tano wa Afrika kupokea Tuzo hiyo ambayo kwa lugha ya Kiingereza inajulikana kama Food Security Policy Leadership Award tokea kuanzishwa kwa Tuzo hiyo mwaka 2008 wakati ilipotolewa kwa aliyekuwa Rais wa Malawi, Hayati Bingu Wa Mutharika.

Viongozi wengine ambao wamepata kutunukiwa Tuzo hiyo ni Rais Armando Emilio Guebuza wa Mozambique mwaka 2009, Rais Hifikepunye Pohamba wa Nambia mwaka 2010 na Malkia, Mama wa Mfalme Ntombi, Indlovukazi wa Swaziland.


Mkutano huo wa mwaka wa FANRPAN unahudhuriwa na wajumbe 249 kutoka nchi 23 zikiwamo 16 ambazo ni wanachama wa taasisi hiyo ambazo ni pamoja na Tanzania, Angola, Botswana, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Lesotho, Mauritius, Mozambique, Kenya, Madagascar, Malawi, Namibia, Swaziland, Afrika Kusini, Uganda, Zambia na Zimbabwe.

Akizumgumza kabla ya Rais Kikwete kukabidhiwa Tuzo hiyo, Mtendaji Mkuu wa FANRPAN, Dkt. Lindiwe Majele Sibanda alimwelezea Rais Kikwete kuwa ni bingwa mtetezi na kiongozi shupavu wa sekta ya kilimo katika Tanzania na Barani Afrika.

Alisema mama huyo: “Mheshimiwa Rais wewe ni bingwa. Unatanguliza mahitaji ya watu wako mbele kama vile unavyofanya katika sekta ya kilimo ambayo ni tegemeo la watu wengi katika Tanzania na Bara letu. Kupitia mipango yako ya kilimo, kamwe Tanzania haitakuwa ile ile ambayo uongozi wake uliupokea mwaka 2005. Kamwe Tanzania imebadilika sana chini ya uongozi wako.”

Dkt. Sibanda aliongeza: “Kwa hakika umefanya mengi siyo kwenye kilimo tu, bali kwenye kusimamia amani na usalama, katika kukuza uhuru wa kila aina, katika masuala ya afya, elimu, miundombinu na maendeleo ya vijana.”

Hata hivyo, Dkt. Sibanda alitoa changamoto tatu kwa Rais Kikwete ambazo ni kumtaka aongeze maradufu matumizi ya mbolea kwa wakulima kutoka kilimo kilo 10 za sasa kwa hekta moja hadi kufikia kilo 25 ifikapo mwaka 2015.

Aidha alimtaka Rais Kikwete kuhakikisha kuwa anaongeza maradufu uzalishaji wa mazao ya kilimo na hasa kuhakikisha kuwa Tanzania inajitosheleza kwa sukari ifikapo mwaka 2015 na tatu kuwashirikisha wakulima wadogo katika uzalishaji mbegu. “Tutarudi tena  Mheshimiwa Rais mwaka 2015 kuyatazama tena upya mambo haya matatu.”

Akizungumza mara baada ya kupokea Tuzo hiyo, Rais Kikwete aliwapitisha washiriki wa mkutano huo kwenye hatua zote ambazo Serikali yake inachukua kupambana na changamoto zote zinazokifanya kilimo cha 

Tanzania kubakia kwenye uduni ikiwa ni pamoja na kuongeza maeneo ya umwagiliaji, matumizi ya mbegu bora, matumizi ya madawa ya kuua wadudu, matumizi ya mbolea nyingi zaidi, uboresha wa miundombinu ya barabara vijijini, uimarishaji wa vikundi vya ushirika wa uzalishaji na upanuzi na uimarishaji wa masomo.

Aidha, Rais aliwaambia wajumbe wa mkutano huo kuwa Serikali yake iko mbioni kuanzisha Soko la Mazao (Commodity Exchange) kama namna ya kuwawezesha kwa uhakika wakulima kwa kuhakikisha wanapata bei nzuri ya mazao yao.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

6 Septemba, 2012

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI ALIUNDA
KAMATI SIO TUME


Wizara
ya mambo ya Ndani ya Nchi inapenda kutoa taarifa kwa Umma kuwa katika kikao
chake na Waandishi wa Habari cha tarehe 4 Septemba, 2012, Waziri wa Mambo ya
Ndani ya Nchi, Dk. Emmanuel Nchimbi alitoa taarifa ya kuunda Kamati
kuhusiana na vurugu zilizotokea katika Kijiji cha Nyololo, wilayani
Mufindi, tarehe 2 Septemba, 2012 ambapo katika vurugu hizo mwandishi wa habari
wa Channel Ten, Daudi Mwangosi alipoteza maisha.

Waziri
Nchimbi alisema aliunda Kamati hiyo,
(na siyo Tume), ili kumsaidia kupata majibu ya maswali yafuatayo, ambayo
alisema hakuwa na majibu yake:

1.     Nini
kilikuwa chanzo cha kifo cha mwandishi wa habari, Bw. Daudi Mwangosi,

2.     Kama
upo uhasama kati ya waandishi wa habari wa Iringa na Polisi,

3.     Kama
ipo orodha ya waandishi watatu (3) waliopangwa kushughulikiwa na Polisi,

4.     Kama
ukubwa wa nguvu za Polisi zilizotumika ulikuwa sahihi,

5.     Kama
zipo taratibu zinazoruhusu Vyama vya Siasa kukata rufaa visiporidhika na
maamuzi ya Polisi,

6.     Kama
kuna tatizo la mahusiano kati ya Polisi na Vyama vya Siasa.

Taarifa
hii inatolewa ili kuweka sawa taarifa zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya
habari vikimnukuu Mkurugenzi wa Masuala ya Sheria, Katiba na Haki za Binadamu
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tindu Lissu akisema Chama chake
hakiungi mkono Tume ya mauaji ya aliyekuwa Mwandishi wa Habari wa Kituo cha
televisheni cha Channel Ten, kwa madai kwamba imeundwa kinyume cha Sheria ya Tume
za Uchunguzi ya Mwaka 1962 Sura ya 29, ambayo alisema kwa mujibu wa Sheria
hiyo, tume zote za uchunguzi huundwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.

Kupitia
taarifa hii, tunapenda kuuarifu Umma kuwa Waziri Nchimbi hakuunda Tume ila
aliunda Kamati hiyo kwa Mamlaka aliyonayo kama Waziri na uundaji wa Kamati hii
hauhusiani kwa vyovyote na matakwa ya Sheria ya Tume za Uchunguzi, Sura ya 32,
Marejeo ya Mwaka 2002.

Utaratibu
wa kutumia Kamati kutafiti jambo kwa kina kwa ajili ya kumshauri Waziri au
kiongozi mwingine yoyote ni wa kawaida katika utendaji na utekelezaji wa
majukumu ya umma.




Imetolewa
na  Isaac J. Nantanga


Msemaji
wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi


06
Sepemba, 2012

Moja Wa Vilabu Vya Waandishi Wa Habari Tanzania Yatoa Tamko Kuhusiana Na Mauaji Ya Mwandishi Daudi Mwangosi Mkoani Iringa

Wajumbe wa Mkutano Mkuu UTPC wakiwa wamesimama kwa dakika moja kumuombea Marehemu Daudi Mwangosi aliefariki katika Vurugu za Chadema na Polisi mkoani Iringa

UMOJA wa Vilabu vya Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC)umesema kuwakufuatia mauaji ya  mwandishi wa habari wa Wa kituo cha Channel Ten Mkoani Iringa Bw. Daudi Mwangosi kimeitaka serikali kuwasimamisha kazi askari waliohusika katika tukio la mauaji ya kinyama ya mwandishi huyo. Umoja huo umesema kuwa askari walioshiriki katika oparesheni hiyo ambayo ni haramu kusimamishwa mara moja ili kupisha uchunguzi kufanyika.

Hayo yalisemwa jana Jijini Dar Es Salaam na Rais wa UTPC Bw.Keneth Simbaya wakati alipokuwa akitoa tamko Kwa Viongozi wa Vilabu Mikoani kuhusiana na mauaji dhidi ya mwandishi wa habari Huyo aliyeuwawa akiwa mikononi mwa polisi katika kijiji cha Nyololo Wilayani Mufindi. “Hapa tunataka uchunguzi huu ukikamilika tunaitaka serikali kuutangazia umma na kupisha sheria kwa wale watakaobainika kuhusikakwa uzembe huo kwa namna moja au nyingine wachukuliwe hatua dhidi ya mauaji hayo ya mwandishi wa habari Bw. Daudi Mwangosi”alisema.

Hata hivyo Bw. Simbaya alisema wakati uchunguzi ukiwa unaendelea serikali iridhie na kurasimisha malipo kwa ajili ya Mjane wa mwandishi huyo na watoto walioachwa na marehemu ili waweze kujikimu.

Aidha alisema licha ya kutoa tamko hilo wanaendelea kulitazamia jeshi la polisi kama mdau mwenye shaka kwa namna wanavyotenda kazi zao na waandishi wa habari mikoani na kwamba watataarifu umma kuhusu
mwenendo wao hapo baadae. “Lakini pia katika mkutano huu tumeridhia kushirikiana na taasisi zingine za haki za binadamu ,uwakili na Utetezi ili kubaini namna bora ya kuishitaki serikali kama mwenendo wa suala hili hautakuwa unaleta tija Kutokana na vithibitisho hivyo tunakaribisha mashirika ya haki za binadamu ,asasi zisizokuwa za kiserikali ili kuweza kufanikisha azma hii”alisema Bw. Simbaya.

Akizungumzia kuhusu usalama kwa waandishi wa habari Bw. Simbaya alisema katika kuhakikisha kuwa waandishi wa habari wanafanya kazi yao kwa usalama amelitaka jeshi la polisi kutoa utaratibu ambao utawezesha wanahabari nchini kufanya kazi kwa usalama bila hofu wala dharau,kutoa elimu kwa jeshi la polisi kuhusu umuhimu wa wanahabari na jukumu lao katika Taifa.

Hata hivyo baadhi ya viongozi wa Vyama vya waandishi wa habari Tanzania ambao wanahudhulio mkutano mkuu wa UTPC walisema tamko hilo halijapewa uzito kutokana na tukio la mauaji lenyewe na jinsi lilivyo huku wakitaka Tamko hilo kupewa uzito wa kina.

 “Hili Tamko lilitakiwa kupewa uzito sana kwani sisi tuliokuwepo katika msiba huo kwa ujumla inasikitisha sana hivyo tamko ni muhimu lipewe uzito zaidi kulingana na mauaji yenyewe yanavyotisha hivyo tufuate maamuzi ya viongozi wa clabu waliotoa matamko ya kususia habari za polisi mpaka pale watakapokuwa wameridhia kukaa meza moja na wanahabari juu ya mauaji hayo”alisema mmoja wa viongozi wa clabu za waandishi wa habari Tanzania Bw. Christopher Nyenyembe.

                 Habari na Esther Macha Na Mwajabu Kigaza

THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali Davis Mwamunyange salamu za rambirambi kuomboleza kifo cha Luteni Kanali (mst) Adam Hussein Mwandu Makwaia, aliyekuwa Mpambe wa Rais wa kwanza wa Tanzania, Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere na Rais Ali Hassan Mwinyi.

Katika salamu zake, Rais Kikwete amemwambia  Jenerali Mwamunyange: “Nimepokea kwa majonzi na masikitiko taarifa za kifo cha Luteni Kanali Makwaia ambaye nimejulishwa kuwa alipoteza maisha Jumanne, Septemba 4, mwaka huu, 2012, katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo mjini Dar es Salaam.”

“Katika miaka yote ya utumishi wa Jeshi na utumishi wa umma, Luteni Kanali Makwaia alikuwa mwadilifu na mwaminifu kwa nchi yake, alikuwa na weledi wa kiwango cha juu katika taaluma yake ya kijeshi na alikuwa mtiifu kwa viongozi wake. Nakutumia wewe Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi salamu zangu za rambirambi kufuatia kifo hiki,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:

“Aidha, kupitia kwako natuma salamu za pole nyingi kwa familia ya marehemu Makwaia ambao wamempoteza baba na mhimili wa familia. Pia, kupitia kwako, natuma salamu za rambirambi kwa maofisa na wapiganaji wote wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambao wamempoteza ofisa na mpiganaji mwenzao.”

Luteni Kanali (mst) Makwaia alijiunga na Jeshi Machi 24, mwaka 1974, na alilitumikia kwa miaka 23 na miezi tisa kabla ya kustaafu. Alikuwa Msaidizi wa Mpambe wa Rais kati ya mwaka 1978 na 1981 na kuwa Mpambe wa Rais kwa miaka sita hadi 1987. Amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 62.

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.

6 Septemba, 2012