Kama ilivyo ada KASIBANTE FM REDIO walirusha laivu kila kitu
Zawadi kwa wadhamini wa mkutano huo nazo zilitolewa.
Pale kati nini washiriki wakisikilizia
Mhe.Meya wa manispaa ya bukoba ANATORY AMANI akiwa katika pozi la kuchati na wenzie.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mkutano mkuu wa 11 wa LVRLAC
Halmashauri za Miji na Wilaya zinazozunguka Ziwa Victoria, zimeshauriwa kushirikisha jamii katika mipango ya hifadhi mazingira, kwa lengo la kuifanya iwe endelevu.
Mkuu wa mkoa wa KAGERA, kanali mstaafu FABIAN MASSAWE, ametoa ushauri huo wakati akifungua Mkutano wa 11 wa Umoja wa Halmashauri 130 kutoka UGANDA, KENYA na TANZANIA,- LVRLAC.
Katika hotuba yake ya ufunguzi kwa niaba ya rais JAKAYA KIKWETE, kanali MASSAWE amesisitiza ushirikishwaji na uwazi kuwa ni mambo muhimu katika utekelezaji wa mipango mbalimbali ya maendeleo.
Aidha, ameonya kuwa juhudi za pamoja zinahitajika kulinda raslimali za Ziwa Victoria, ambazo zinatoweka kwa kiwango cha kutisha kutokana na uharibifu wa mazingira.
Amesema kuwa vitendo vya uvuvi haramu na matumizi ya zana haramu vinazidi kuongezeka na kutishia uhai wa ziwa hilo.
Ameonya kuwa endapo hatua za dhati hazitachukuliwa, kuna hatari ya Ziwa hilo kutoweka katika uso wa dunia.
Takriban Washiriki 450 wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri, Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri 28 za Tanzania wamehudhuria Mkutano huo, ambao umefanyika katika viwanja vya GYMKHANA, katika Manispaa ya BUKOBA.
