maporomoko

maporomoko

Saturday, August 4, 2012

MAADHIMISHO YA MIAKA 100 YA HOSPITALI YA KAGONDO








Rais wa mashirika ya kipapa ya kimisionari duniani askofu Protase Rugambwa amewataka  wananchi mkoani Kagera kuchangia miradi mbalimbali ya maendeleo husani miradi inayohusu suala la afya .
Askofu Rugambwa ametoa wito huo katika maadhimisho ya miaka 100  ya hospirtali ya kagondo tangu kuanzishwa kwa yaliyofanyika leo hospitalini hapo wilayani muleba.
Amesema kila mwananchi mwenye nguvu za kufanya kazi anatakiwa wawe wa kwanza katika kuchangia kabla  serikali haijaweka mkono ili kuonesha uungaji mkono jitihada za serikali.

Akisoma risala kwa mgeni rasmi  mganga mkuu wa hospitali hiyo Dk.modest Lwakahemla amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 100,hodspitali hiyo imehakikisha inaondoa  tatizo la ukosefu wa vitanda ambapo kwa sasa ina uwezo wa kulaza wagonjwa 160.
Aidha ameongeza kuwa licha ya mafanikio hayo hospitali imeweza kuingia mkataba na madaktari bingwa kutoka nchi za nje ili kuimariosha huduma za kiafya hospitalini hapo.
 NA  junior mwermezi

No comments:

Post a Comment