maporomoko

maporomoko

Wednesday, August 29, 2012

Rais wa Senegal ataka Bunge la Senate lifutwe ili fedha itumike kuokoa maisha ,

Rais wa Senegal, Macky Sall ametoa wito wa kufutiliwa mbali kwa bunge la Senate, huku pesa ambazo hutumika kulipia shughuli za bunge hilo akiagiza zitumike kwa msaada wa chakula.

Rais huyo ametoa agizo hilo baada ya kukatiza ziara yake nchini Afrika Kusini ili kushugulikia mafuriko makubwa yaliyoikumba nchi hiyo na kusababisha vifo vya watu 13.

Akiongea katika uwanja wa ndege wa Dakar rais Macky Sall, amesema kuwa atawasilisha mwaada huo wa dharura bungeni ili kufutilia mbali bunge la Senate.

amesema kiasi cha pesa Pesa ambazo hutumiwa na bunge hilo ni takriban dola milioni 15, ambazo zitaweza kutumika kuzuia na kuwasaidia waathirika wa  mafuriko kwa siku za usoni.

Ingawa maeneo ya nyanda za chini nchini Dakar hukumbwa na mafuriko kila msimu wa mvua, mwaka huu athari zimekuwa kubwa kwa sababu ya mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mengi ya Afrika Magharibi ambapo Inakisiwa kuwa maelfu ya watu wameachwa bila makao.

Hapo awali, wananchi walifanya maandamano kutuhumu serikali kwa kushindwa kuchukua hatua mbadala za kukabiliana vilivyo na hali hiyo ya mafuriko ingawa walitawanywa na gesi ya kutoa machozi.

Mwezi Mei mwaka huu, Benki ya Dunia iliahidi kutoa dola milioni 55.6 ili kuweza kuimarisha miundo mbinu itakayowezesha nchi hiyo kukabiliana na mafuriko.

Nchi hiyo imekuwa mfano mzuri wa nchi yenye demokrasia barani Afrika ikiwa na mfumo mzuri wa siasa za vyama vingi na mfumo wa majimbo.

SOURCE WAVUTI..

No comments:

Post a Comment