
Wanajeshi wakisindikiza mwili wa John Atta Mills
Maelfu ya wananchi wa Ghana jijini Accra wamehudhuria mazishi ya kitaifa ya rais John Atta Mills aliyefariki ghafla mwezi Julai mwaka huu.
Mills aliyeugua saratani ya koo kwa muda mrefu amefariki ikiwa imebaki miezi mitano tu kabla ya kufanyika uchaguzi wa urais ambao angegombea tena nafasi hiyo.
Mwandishi wa BBC mjini Accra anasema kifo chake kimewaunganisha Waghana katika majonzi.
Anasema kifo hicho kilionekana kama jaribio kwa demokrasia changa ya nchi hiyo.
Mills aliyeanza kipindi cha miaka minne ya urais mwezi Januari mwaka 2009, amerithiwa na makamu wake rais John Dramani Mahama.
Ghana imepongezwa na jumuiya ya kimataifa kwa namna ambavyo imeshughulikia kipindi cha mpito katika taifa hilo linalofahamika kwa siasa zake za mgawanyiko.
Waombolezaj katika mazishi ya John Atta MillsAmefanya mazungumzo na rais Mahama.
Ikionekana kama mfano bora wa demokrasia katika eneo hilo la Afrika, ghana ilichaguliwa na rais wa Marekani Barack Obama katika ziara yake ya nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara mwaka 2009.
Mills aliyefariki akiwa na umri wa miaka 68 alikuwa ni mwanasiasa wa ngazi ya juu kwa miaka mingi.
Kati ya mwaka 1997-2001 alikuwa makamu wa rais kwa aliyekuwa mtawala wa kijeshi Jerry Rawlings, lakini alijiweka mbali na kiongozi huyo.
Aliingia madarakani baada ya ushindi mwembamba dhidi ya mgombea kutoka kilichokuwa chama tawala cha New Patriotic Party, Nana Akufo-Addo
katika uchaguzi wa mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment