maporomoko

maporomoko

Saturday, August 11, 2012

WATAALAMU WA AFYA WASEMA EBORA SASA KWISHINE.

Shirika la msaada wa matibabu la nchini uganda maarufu kama  MSF, linasema kuwa ugonjwa  wa virusi vya Ebola, uliozuka nchini Uganda ambao kwa sasa hivi unaonekana kuwa hatari kwa wakazi wa jiji la mwanza ambapo watu watano wanaohisiwa kuambukizwa na virusi hivyo , unaonesha kuwa umedhibitiwa.
Ebola Uganda
Akizungumza na kagera amani na maendeleo afisa mmoja wa MSF anayeshghulika na magonjwa yanayoambukiza, Dr Paul Roddy, alisema kifo cha mwisho kilichosababishwa na Ebola kilitokea siku 11 zilizopita.

Lakini alionya kwamba iwapo kuna virusi eneo fulani ambavyo bado havikushughulikiwa, ugonjwa unaweza kujitokeza tena.
Alisema imethibitishwa kuwa vifo 19 vilitokana na ugonjwa uliotokea kwenye mji wa Kagadi.

Dr Roddy alisema inawezekana virusi hivo vilitokana na popo, ambao pengine waliwaambukiza nyani - nyama ya nyani huliwa na wawindaji.

No comments:

Post a Comment